Madrid yatakata kwa kuwachapa La Palmas

Madrid

Chanzo cha picha, Google

Maelezo ya picha,

Marco Asensio na Marcelo wakingalia goli

Ligi kuu ya nchini Hispania La Liga imendelea tena mwisho wa wiki Real Madrid wakicheza katika dimba la nyumbani Santiago Bernabeu wameshinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Las Palmas.

Magoli ya Real Madrid yalifungwa na Casemiro, alianza kufunga goli la kwanza kisha Marco Asensio akaongeza goli la pili na Isco akafunga goli la tatu.

Manyambizi Villarreal wakautumia vyema uwanja wao wa De la Ceramica kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 kwa kuwafunga Malaga.

Matokeo ya michezo mingine ya La liga

Levante 1 - 2 Girona

Celta Vigo 3 - 1 Athletic Bilbao

Real Sociedad 3 - 1 Eibar