Dionatan Teixeira: Beki wa zamani wa Stoke afariki akiwa na miaka 25

Dionatan Teixeira

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Teixeira aliumia mguuni msimu wake wa kwanza Stoke kabla ya mkataba wake kutamatishwa Januari

Beki wa zamani wa Stoke City Dionatan Teixeira amefariki dunia akiwa na miaka 25 kutokana na kile akinachoaminika kuwa mshtuko wa moyo.

Alijiunga na Stoke 2014 baada ya kufanyiwa majaribio klabu kadha za Ligi ya Premia ikiwemo Manchester City.

Lakini mchezaji huyo wa Brazil hakufanikiwa England kwani alitatizwa na majeraha.

Alichezea Stoke mechi mbili pekee, kama nguvu mpya katika miaka mitatu aliyokaa Stoke.

Teixeira alikuwa Brazil alipougua na kufariki Jumapili, kwa mujibu wa klabu yake aliyokuwa anaichezea FC Sheriff, ya Moldovia ambayo inacheza ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League msimu huu.

Klabu hiyo ilishinda ligi nchini humo pamoja na kombe la ligi.

FC Sheriff wamesema: "Atasalia daima katika nyoyo zetu."