Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 06.11.2017

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption David Silva

Liverpool wana mpango wa kumwinda mchezaji wa kiungo cha kati wa Uhispania na Manchesert City David Silva, 31. (Sun)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte ambaye awali alikuwa anaiongoza Juventus, ametupilia mbali ripoti zinazomhusisha na AC Milan. (Daily Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption David Luiz

Mlinzi wa Chelsea na Brazil David Luiz aliachwa nje ya kikosi kilichoishinda Manchester United bao 1-0 baada ya mchezaji huyo kutilia shaka mbinu za maandalizi za Conte kabla ya mechi. (Times - subscription required)

Meneja wa Watford Marco Silva amekataa kujibu maswali kuhusu kazi huko Everton baada ya kblabu yake kushindwa 3-2 na Everton. (Liverpool Echo)

Arsenal na Manchesetr City wanatarajiwa kumwida mchezaji wa safu ya kati wa Ajax, Frenkie de Jong, 20, mwezi Januari. (Sun)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Riyad Mahrez

Roma wanasema kuwa wao na Barcenoa walikuwa na nia ya kumsaini wing'a wa Leicester Riyad Mahrez, 26, lakini hakuna mwenye alikuwa tayari kulipa pauni milioni 50 iliyokuwa ikiombwa na mchezaji huyo. (Daily Mirror)

Meneja wa West Brom Tony Pulis hana hofu kuwa mechi kumi bila ushindi na kushindwa mara tatu mfululizo kutasababisha bodi klabu hiyo kumfuta. (Birmingham Mail)

Aston Villa hawana mpango wa kuwauza Scott Hogan, 25, Henri Lansbury, 27, Jack Grealish, 22, au James Bree, 19 ambao wote wamehusishwa na kuondoka huko Villa Park.

Mada zinazohusiana