Kane na Winks waondolewa kikosi cha England

England

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Harry Keane na Harry Winks wote waliumia katika mchezo wa ligi dhidi ya Crystal Palace

Wachezaji wawili wa klabu ya Tottenham mshambuliaji Harry Kane na kiungo Harry Winks wameondolewa kwenye timu ya taifa ya England sababu ya kuwa majeruhi.

Harry Kane anasumbuliwa na maumivu ya goti huku Winki akiwa na tatizo la kifundo cha mguu na hivyo wachezaji hawa watakosa michezo miwili ya kirafiki ya timu ya taifa ya England.

Kiungo wa klabu ya West Bromwich Albion Jack Livermore, pamoja na beki Michael Keane wameitwa ameitwa kuziba mapengo ya wachezaji hao

England itacheza na Ujerumani mchezo wa kirafiki siku ya ijumaa na kisha Brazil jumanne ijayo mchezo yote ikichezwa katika dimba la Wembley.