Khune huenda akakosa mchezo wa kufuzu kombe la dunia

Khune

Chanzo cha picha, Google

Maelezo ya picha,

Kipa wa Afrika Kusini Itumeleng Khune

Kipa wa timu ya taifa ya Afrika kusini Itumeleng Khune huenda akakosa michezo miwili muhimu ya kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia dhidi ya Senegal.

Kipa huyo aliumia mfupa wa karibu na jicho la kulia wakati timu yake ya Kaizer Chief ilipocheza na Chippa United.

Khune alipelekwa Hospitali na kufanyiwa uchunguzi na taarifa ya klabu yake imeeleza anaweza kuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja mpaka wiki sita kama kutakuwa na haja ya kufanyiwa upasuaji.

Afrika kusini watacheza na Senegal siku ya ijumaa katika mchezo wa kuwania kufuzu na ni lazima kushinda mchezo huo ili kupata nafasi ya kwenda Urusi mwakani.