Mkufunzi wa West Ham abwaga manyanga

Mkufunzi wa West Ham abwaga manyanga

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mkufunzi wa West Ham abwaga manyanga

Mkufunzi wa West Ham Slaven Bilic amefutwa kazi huku kocha wa zamani wa Everton na Manchester United David Moyes akitarajiwa kuchukua mahala pake kwa muda.

Bilic mwenye umri wa miaka 49 aliichukua timu hiyo ilipokuwa katika eneo hatari la kushushwa daraja katika jedwali la ligi ya Uingereza.

Mechi yake ya mwisho ilikuwa kichapo cha 4-1 dhidi ya Liverpool katika uwanja wa London.

West Ham ilisema klabu hiyo inaamini mabadiliko ni muhimu kusonga mbele kutokana na ndoto yake.

Moyes ambaye alisema kwamba yuko tayari kuuchukua wadhfa huo ameorodheshwa kuchukua kazi hiyo hadi mwisho wa msimu huu.