David Moyes ndiye kocha mpya wa West Ham

Mkufunzi mpya wa West Ham David Moyes
Maelezo ya picha,

Mkufunzi mpya wa West Ham David Moyes

Mkufunzi wa zamani wa Everton na Manchester United david Moyes amechukua mahala pake Slaven Bilic, ambaye alifutwa kazi siku ya Jumatatu wakati klabu hiyo ikiwa katika nafasi ya kushushwa daraja.

Moyes amekuwa bila kazi tangu mwezi Mei wakati alipojiuzulu kama mkufunzi wa Sunderland baada ya klabu hiyo kushushwa daraja.

Mwenyekiti mwenza wa West Ham David Sullivan alisema kuwa mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 54 raia wa Uskochi ndio mtu anyefaa kurithi nafasi hiyo.

Aliongezea: Tunahitaji mtu mwenye uzoefu ,utambuzi wa ligi ya Uingereza na wachezaji wake na tunaamini kwamba David anaweza kuwaimarisha wachezaji.

Ni mtu anayeheshimika katika soka na ataleta motisha na mawazo mapya.

Alithibitisha na Everton kwamba ana uwezo na tunadhani kwamba West Ham ni klabu ambayo itampatia fursa David Moyes kuonyesha uwezo wake.

Mechi ya kwanza ya Moyes itakuwa dhidi ya Watford katika ligi ya Uingereza mnamo mwezi Novemba 19.