Ligi Kuu England: Kwa nini itakuwa vigumu kuwafikia Manchester City

Sergio Aguero and Leroy Sane Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sergio Aguero na Leroy Sane

Manchester city wameshinda michezo 15 mfululizo kwenye mashindano yote msimu huu, wakiongoza ligi ya Uingereza kwa alama nane.

City walikwea zaidi kileleni baada ya kuichapa Arsenal 3 - 1 kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Ethiad siku ya Jumapili kabla ya Manchester United kupoteza dhidi ya Chelsea, City kwa sasa ni kama hawazuiliki

Alan Shearer anaamini kinachozinyima usingizi timu nyingine kwenye mbio hizo za ubingwa ni namna ambavyo City wameimarika toka walipomaliza msimu uliopita wakiwa nyuma ya mabingwa Chelsea kwa alama 15 kwenye msimu wa kwanza wa kocha Pep Guardiola kukinoa kikosi hicho.

City wanazidi kusonga mbele wakiwa na magoli 38 kutoka kwa michezo 11 ambayo wameshacheza msimu huu wanonekana kuimarika sana katika safu ya ushambuliaji na ulinzi.

Katika mchezo na washika mitutu wa London golikipa Ederson aliokoa mkwaju wa Aaron Ramsey ambao ulikuwa unatokomea kimiani, wachambuzi wanasema msimu uliopita wakiwa na golikipa Claudio Bravo bila shaka mkwaju huo ungekuwa goli

Na kama ungetinga wavuni ingekuwa 1-1 badala ya 1-0 na matokeo hayo yangeweza kabisa kubadili hali ya mchezo

Inaonekana Pep Guardiola amejifunza kutokana na makosa waliyoyafanya msimu ulipita kiasi cha kuwa tishio kwa vilabu vingine msimu huu

Alan Shearer anasema ailipokuwa Blackburn, Manchester United walikuwa wakiongoza kwa alama 12 baaada ya michezo 16 ya msimu wa 1993 - 94 lakini walilipambana na kuwafikia kufikia mwezi Aprili.

Sita bora Ligi ya Premia
Klabu Mechi Tofauti ya mabao Alama
Manchester City 11 +31 31
Manchester United 11 +18 23
Tottenham Hotspur 11 +13 23
Chelsea 11 +9 22
Liverpool 11 +4 19
Arsenal 11 +4 19

Lakini tatizo kwa timu nyingine ni kwamba Shearer haoni udhaifu wowote kwa City, walipocheza na Arsenal kwa kifupi msimu huu wamo kwenye kiwango kizuri sana.

Katika misimu miwili iliyopita City walizanza vizuri pia, lakini wakati wa kipindi cha baridi walitetereka, pengine kutokana na majeruhi na mpangilio wa ratiba lakini Guardiola anajua hawezi kuruhusu hilo lifanyike tena.

Ameshinda mataji akiwa Uhispania na Ujerumani kama mwalimu anajua nini chakufanya, kwa sasa ana kikosi kamili ata akiwa na majeruhi ana mbadala wa kutosha kuliko timu nyingine yoyote msimu huu.

Aguero asipokuwepo, wana Jesus

Sergio Aguero akiumia wana Gabriel Jesus wakati Chelsea bila Alvaro Morata wata yumba Tottenham bila Harry Kane, Manchester United bila Romelu Lukaku watashuka.

Utangulizi wao kwa alama nyingi unatisha klabu nyingine.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii