Sadio Mane: Mchezaji aliyewafaa sana Liverpool

Sadio Mane

Nyota wa Senegal na Liverpool Sadio Mane alifanya vizuri sana mwaka 2017 hivi kwamba alipigiwa kura na wachezaji wenzake kuwa kwenye kikosi bora cha PFA.

Kadhalika, alikuwa mmoja kati ya Waafrika wawili kuteuliwa kushindania tuzo ya Ballon d'Or.

Pia alitekeleza wajibu mkubwa katika kuiongoza Senegal kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 2002.

Katika ufungaji wake bora zaidi akiichezea Senagal mwaka mmoja, Mane alifunga mabao manne katika mechi 9 za kimataifa.

Ilikuwa ni tofauti sana na mwanzoni mwa mwaka kwani Mane alionesha ukakamavu wake kiasi cha kufikia kasi yake ya umeme, ujanja wake na ustadi wa kutia mabao kimiani.

Baada ya kufunga katika mechi za kwanza mbili hatua ya makundi katika mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika, mwaka wa Mane ulibadilika na kuwa mchungu.

Alishindwa kufunga mkwaju wa penalti wakati wa mikwaju ya kuamua mshindi dhidi ya Cameroon na akawawezesha samba hao ambao baadaye waliibuka mabingwa kufika hatua ya nne bora. Hilo lilimdhoofisha sana Mane, machozi yakionekana kutiririka kama maji kwenye uso wake siku hiyo.

Liverpool bila shaka walifurahia sana sana jinsi mshambuliaji huyo raia wa Senegal alivyojikwamua, kwa sababu walishinda tu mechi moja bila yeye kutokuwepo katika mechi saba ambapo pia waliondolewa katika michuano miwili ya kushindania vikombe.

Alichangia ushindi wa kwanza wa Liverpool tangu aondoke kwenda Gabon na kufunga mabao mawili ya Liverpool dhidi ya Tottenham kwenye ushindi wao wa 2-0 kabla ya kufunga dhidi ya Arsenal na pia mahasimu Everton (ambapo Mane alifunga ugenini na nyumbani).

Huwezi kusikiliza tena
AFOTY 2017: Wasifu wa Sadio Mane

Alimaliza msimu wake na mabao 13, ambayo yalikuwa ni matokeo bora Zaidi kwake Ligi ya Premia, licha kukosa mechi za Aprili na Mei baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye goti.

Hata hivyo, Mane bado alimaliza msimu wake wa kwanza Liverpool akiwa anashikilia pamoja na Coutinho nafasi ya mfungaji bao bora klabu hiyo.

Hii ni licha ya kwamba alicheza mechi chache akilinganishwa na Mbrazil huyo.

Aliwasaidia Liverpool kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka minane.

Alitawazwa pia Mchezaji Bora wa Liverpool wa Msimu na pia Mchezaji Bora wa Msimu chaguo la Wachezaji.

Kufikia wakati ambao alionyesha kadi nyekundu kwa njia yeye utata dhidi ya Manchester City msimu mpya Septemba baada ya ligi mpya kuanza, ambapo alianza kwa magoli matatu katika mechi tatu, Liverpool walikuwa wanachezea mabao 2:2 ligini wakiwa na Mane kikosini - ikilinganisha na 1.6 akiwa hayupo.

Ukizingatia ni kwa kiwango gani mshambuliaji huyo wa miaka 25 alikoswa na Liverpool, umuhimu wake huonekana wazi zaidi wakati Mane hayuko uwanjani. Na nyota huyo Msenegali ana matumaini ya kushinda tuzo la mchezaji bora wa BBC wa mwaka mara yake ya tatu kushindania.

Mada zinazohusiana