Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 13.11.2017

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Lionel Messi

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi anatakana klabu hiyo kumtafuta mchezaji wa kiungo cha kati wa Tottenham Dele Alli, 21, kabla ya Real Madrid hawajafanya hivyo. (Don Balon - in Spanish)

Mshambuliaji wa Atletico Madrid Fernando Torres, 33, ana nia ya kurejea Premier League huku Southampton na Newcastle wakitaka kumsaini. (Daily Mirror)

Manchester United wako tayari kulipa pauni milioni 177 kumsaini mchezaji wa kati wa Real Madrid Marco Asensio, 21. (Don Balon - in Spanish)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Marco Asensio

Manchester United wanataka kumuuza mchezaji wa England Luke Shaw ,22, kwa karibu pauni milioni 20 mwezi Januari. (Times - subscription required)

Manchester City na Juventus wanatamka mchezaji wa kati wa Liverpool Emre Can, 23, ambaye mkataba wake utakwisha msimu huu. (Daily Star)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Patrice Evra

Patrice Evra amezungumza na vilabu kadha vinavyotaka kumsaini licha ya kumvamia shabiki wa Marseille kwa mujibu wa ajenti wake. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Mshambuliaji wa West Ham Marko Arnautovic, 28, anasema hatauzwa mwezi Januari. (Kurier - in German)

Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 31, anasisitiza kuwa atakuwepo kwenye klabu hiyo. (Independent)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Olivier Giroud

LiverpooL wanataka kutumia paunia milioni 5 kumsaini mchezaji wa miaka 17 wa Wolves Morgan Gibbs-White mwezi Januari. (Sun)

Wolves wamemuahidi meneja Nuno Espirito Santo pesa zaidi kumuwezesha kubadili klabu na kuwa mshiriko wa Champions League. (Daily Mirror)