Wamiliki wa Leicester wakana kudaiwa deni la £323m

Wamiliki wa klabu ya Leicester nchini uingereza wamekana kudaiwa deni la £323m na serikali ya Thai.
Image caption Wamiliki wa klabu ya Leicester nchini uingereza wamekana kudaiwa deni la £323m na serikali ya Thai.

Wamiliki wa klabu ya soka ya Leicester City wamesema '' wanapinga bila shaka'' ripoti kwamba wanadaiwa £323m na serikali ya Thai.

Siku ya Jumatatu kwenye mahakama ya jinai huko Bangkok iliripotiwa na shirika la habari la Reuters kwamba walikiri shtaka hilo dhidi ya King Power International.

Hatahivyo , klabu hiyo na King Power wamesema madai hayo '' bado hayajakubalika.''

Wamesema ''watapigana hadi mwisho'' jaribio lolote '' la ''kuwaharibia jina.''

Kesi hiyo inailaumu King Power kwa kukosa kuilipa serikali ya Thai bilioni 14 baht (£323m) katika operesheni ya kufanya biashara bila kulipa ushuru tangu mwaka 2006.

Kesi hiyo pia itawashirikisha wanaomiliki uwanja wa ndege wa taifa wa Thailand, Reuters imesema.

Mahakama hiyo ya jinai huko Bangkok sasa itawasikiliza mashahidi wa kesi hiyo mwaka ujao Februari , Reuters imeongeza.

Mada zinazohusiana