Ndikumana Hamad 'Katauti': Nahodha wa zamani wa timu ya taifa Rwanda afariki

Katauti
Image caption Katauti aliendesha mazoezi kama kawaida jana

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda Amavubi amefariki dunia.

Ndikumana Hamad 'Katauti' alifariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya mjini Kigali.Ndikumana alikuwa kocha msaidizi katika timu yake ya zamani ya Rayon Sports.Msemaji wa timu hiyo Olivier Gakwaya ameiambia BBC kuwa Katauti jana aliendesha mazoezi kama kawaida kabla ya kurejea nyumbani kwake mtaa wa Nyamirambo."Baadaye hakujihisi vizuri akaenda kununua dawa katika duka la dawa lakini lakini hali yake imeendelea kuwa mbaya ndipo amepelekwa hospitali ya CHUK alikofariki," amesema Oliver Gakwaya.Ndikumana alichezea timu ya Rayon Sports na timu ya taifa ya Rwanda kwanzia mwaka 1998 na kuwa nahodha wa muda mrefu wa Amavubi.

Pia alicheza soka la kulipwa ulaya katika timu za Gent na Anderlecht za Ubelgiji, Omonia Nicosia na Limassol za Cyprus.Mwaka 2009 alifunga ndoa na nyota wa filamu ya Tanzania Irene Uwoya maarufu Oprah kabla ya ndoa yao kuvunjika rasmi miaka 3 iliyopita.

Mada zinazohusiana