Francis Kone, mchezaji aliyeshinda tuzo kwa kumuokoa mchezaji mwenzake

Francis Kone ashinda tuzo la kumuokoa mchezaji mwenzake Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Francis Kone ashinda tuzo la kumuokoa mchezaji mwenzake

Mchezaji huyu wa kimataifa wa Togo alizawadiwa zawadi hiiyo ya heshima mwezi mmoja uliopita baada ya kuokoa maisha ya Berkovic wa Bohemians' wakati akicheza ligi ya Czech mwezi wa pili mwaka huu.

Kone alichukua maamuzi ya haraka kumsadia goli kipa huyu baada ya kugongana na mchezaji mwenzake.

Kone aliingiza kidole mdomoni kwake na kumgeuza kuzuia asimeze ulimi wake.

Ijapokuwa hatua alizochukuwa zaweza kuwa tofauti na utaratibu wa huduma za kwanza yalikuwa ni maamuzi ya aina yake yaliyookoa maisha ya mchezaji mwenzake.

Uwepo wa vyombo vya habari ulifanya jina la shujaa huyo kuanza kung'ara.

Image caption Francis Kone mchezaji wa Togo ambaye amekuwa akiokoa maisha ya wachezaji wenzake

Binafsi mchezaji huyo hakutegemea kupokea tuzo hiyo ya mwaka, jina lake liking'ara sambamba na nyota wengine kama akina Cristiano Ronaldo Gianluigi Buffon and Zinedine Zidane wakati wa hafla ya kutoa tuzo hizo mwezi wa kumi mjini London.

''Nilishangaa sana Ilikuwa kama ndoto'', alisema kone aliyezaliwa nchini Ivory cost lakini ameishindia Togo vikombe viwili sababu ya uraia wa mama yake.

Mchezaji huyu mwenye miaka 26 anaamini kuwa tuzo hii itakuwa mwanzo wa kukomeshwa kwa ubaguzi wa rangi.

Mshambuliaji huyu katika dakika 30 za kwanza za mchezo aliandamwa na kelele za kibaguzi za mashabiki wa Bohemian katika mchezo wao wa mwezi wa pili mjini Prague.

''Ni ujumbe ,mchezo wa kiungwana unamaanisha jambo kama hili pia kuacha ubaguzi ni uungwana pia'', alisisitiza nyota huyo.

Anasema hajui viongozi wa timu hiyo walisema nini ila walipiga simu kwa viongozi wa timu yake na kuomba radhi na kusema ahsante sababu alimwokoa mchezaji wao.

Anasema waliomba radhi kwa sababu walimrushia maneno machafu na kumwita majina ya dhihaka kama vile nyani na mengine mengi.

Tukio hilo halikubadilisha mtazamo wa mashabiki wa Bohemians peke yao bali hata jamii nzima nchini humo.

Mchezaji huyu anasema ameshaokoa maisha ya wachezaji wenzake mara kadhaa (2011) Nchini Thailand na Abidjan (2013 and 2015)

Mada zinazohusiana