Southampton 4-1 Everton

Southampton imekwea hadi nafasi ya 10 kwenye orodha ya ligi baada ya kuishinda Everton. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Southampton imekwea hadi nafasi ya 10 kwenye orodha ya ligi baada ya kuishinda Everton.

Matatizo ya Everton chini ya meneja David Unsworth yameendelea kudhihirika wakati wamedidimia katika Ligi ya England kwa kushindwa pakubwa na Southampton.

Mshambuliaji wa Saints, Charlie Austin amefunga magoli mawili kwa kichwa katika nusu ya pili ya mechi hiyo, baada ya Dusan Tadic kuwapa wenyeji Southampton uongozi wa mapema.

Mchezaji wa Everton aliyelipiwa gharama ya juu kuliko mchezaji mwingine katika klabu hiyo Gylfi Sigurdsson alisawazisha mambo kabla ya kipenga cha mapumziko lakini Southampton wakafyetuka kwa kasi baada ya mapumziko hayo.

Baada ya magoli mawili ya Austin, Steven Davis alimchenga Jordan Pickford kutoka ukiongoni mwa boxi kuufunga ushindi kwa Saints, ambaop waliwahi kufunga magoli sita ya msimu huu nyumbani kabla ya mechi ya leo.

Mada zinazohusiana