Bao la lala salama laipa Arsenal ushindi

Alexis Sanchez amefunga bao lake la nne msimu huu na kuipa Arsenal ushindi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alexis Sanchez amefunga bao lake la nne msimu huu na kuipa Arsenal ushindi

Alexis Sanchez amefunga penalti katika muda wa kuyoyoma na kuipa Arsenal ushindi dhidi ya Burnley uwanjani Turf Moor.

Ilikuwa ni marudio ya mechi ya msimu uliokwisha kati ya timu hizo mbili uwanjani Emirates wakati raia wa Chile - Sanchez alipofunga bao kunako dakika 98 kushinda mechi hiyo.

Ilikuwa pia ni mara ya tatu mtawalia kuwa Gunners imepata ushindi katika muda wa mwisho wa mechi dhidi ya Clarets.

Pointi tatu iliyojinyakulia Arsenal inaikweza timu hiyo hadi katika nafasi ya nne kwenye orodha wakati wakisubiria mechi yao dhidi ya wapinzani wao wa Londona kaskazini Tottenham, waliotoka sare ya 1-1 dhidi ya West Brom Jumamosi.

Matokeo hayo yalikuwa ni kipigo kwa upande wa Sean Dyche ikiwa wamefanikiwa ushindi wa mechi zao mpaka sasa ikiwa walionekana kama watanyakuwa japo pointi moja, kabla ya refa Lee Mason kuashiria sehemu ambapo mlinzi James Tarkowski alimsukuma Aaron Ramsey.

Petr Cech ndiyo aliyekuwa na kibarua kigumu kati ya makipa wawili , akifanikiwa kuokoa mikwaju miwili na kumnyima goli Johann Berg Gudmundsson.

Robbie Brady pia alikuwa na 'free-kick' kuelekea kona iliosukumwa kando na Cech.

Mada zinazohusiana