Ufaransa yaichapa Ubelgiji, yashinda kombe la Davis

Wachezaji wa Ufaransa wakishangilia ushindi
Image caption Wachezaji wa Ufaransa wakishangilia ushindi

Ufaransa imefanikiwa kushinda kombe la Davis kwa mara ya kumi katika historia baada ya kuichapa Ubelgiji katika mchezo wa fainali.

Ufaransa walianza kwa ukali na kuongoza kabla ua Ubelgiji kusawazisha kupitia David Goffin lakini Ufaransa ikaongeza makali na kushinda kwa seti 7-6 (7-5) 6-3 6-2.

Ni michuano ambayo watu wengi walidhani Ubelgiji ingejizolea taji hilo kutokana na uonyesha kiwango safi kwa msimu huu.

Mara ya mwisho mwa Ufaransa kushinda taji hili ilikuwa mwaka 2001, na kwa ushindi huu umati mkubwa wa watu 27,000 walijitokea kushangilia kwa kila aina katika uwanja wa Lille.