Gareth Bale kurejea uwanjani leo

Gareth Bale amekua akikumbwa na majeraha ya mara kwa mara
Image caption Gareth Bale amekua akikumbwa na majeraha ya mara kwa mara

Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale atacheza kwa mara ya kwanza siku ya Jumanne baada ya kukaa nje kwa miezi miwili.

Kocha wa Madrid Zinedine Zidane amesema Bale tiyari amepona na kwa sasa yupo tiyari kurejea uwanjani kuongeza nguvu katika kikosi chake ambacho hakionekani kufanya vizuri kama misimu miwili iliyopita.

Bale amekuwa nje kutokana na kupatwa na majereha ya goti na baadae nyonga na kwa sasa amejumuishwa katika timu itakayocheza na Fuenlebrada kwenye kombe la Copa del Rey.

Bale raia wa Wales alionekana mara ya mwisho uwanjani walipoichapa Borussia Dortmund 3-1 kwenye kombe la klabu bingwa Ulaya.

Bale ambaye pia alikosa kucheza wakati timu yake ya Wales ikisaka kufuzu kombe la dunia, hajacheza sambamba na Cristiano Ronaldo ama Karim Benzema tokea kuanza kwa msimu huu kwa sababu ya majereha ama kuwa na adhabu.