Mkufunzi wa Sevilla aliyepatikana na saratani kufanyiwa upasuaji

Mkufunzi wa Sevilla aliyepatikana na saratani kufanyiwa upasuaji Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkufunzi wa Sevilla aliyepatikana na saratani kufanyiwa upasuaji

Mkufunzi wa Sevilla Eduardo Berizzo atafanyiwa upasuaji siku ya Jumanne baada ya kupatikana na saratani ya tezi dume mapema mwezi huu.

Hali ya mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 48 ilitangazwa baada ya kikosi chake kutoka nyuma na kupata sare ya 3-3 dhidi ya Liverpool katika kombe la vilabu bingwa wiki iliopita.

Sevilla inasema kuwa kurudi kwa Berizzo kutategemea muda atakaochukua kupona upasuaji huo.

Naibu mkufunzi wake Ernesto Marcucci ataiongoza timu hiyo kwa sasa.

Berizzo aliteuliwa kuwa mkufunzi wa Sevilla msimu huu kwa kandarasi ya miaka miwili baada ya kuifunza Celta vigo kwa takriban miaka mitatu.

Mada zinazohusiana