Zimbabwe yajitoa mashindano ya Cecafa

Kikosi cha timu ya taifa ya Zimbabwe
Image caption Kikosi cha timu ya taifa ya Zimbabwe

Timu ya taifa ya Zimbabwe imejiondoa kwenye mashindano ya Cecafa yanayotarajiwa kuanza siku ya Jumapili nchini Kenya.

Zimbabwe imetaja sababu kubwa ya kujiondoa kwake kuwa ni usalama.

Zimbabwe na Libya zilialikwa kama mgeni katika mashindano haya ambayo yanazijumuisha nchi za Afrika Mashariki na Kati ikiwemo bingwa mtetezi Uganda, wenyeji Kenya, Tanzania, Rwanda, Zanzibar, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini.

Kocha wa Zimbabwe Sunday Chidzambwa, tiyari alikwisha taja kikosi chake, lakini chama cha soka cha Zimbabwe kikasema kwa sasa hali ya Kenya hairuhusu.

Hali ya usalama ya Kenya bado ni ya kusuasua kufuatia vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu.