Conte asema kuna njama ya mpangilio wa mechi dhidi ya Chelsea

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte asema kuwa kuna njama ya mpangilio wa mechi dhidi ya klabu yake Haki miliki ya picha PA
Image caption Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte asema kuwa kuna njama ya mpangilio wa mechi dhidi ya klabu yake

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte asema kuwa kuna njama ya mpangilio wa mechi dhidi ya klabu yake.

Raia huyo wa Itali awali alinukuliwa akihoji mpangilio wa mechi za ligi ya Uingereza, hususan tofauti ya muda wa kupumzika kati ya klabu yake na wapinzani wake.

Siku ya Jumamosi , Chelsea inaialika Newcastle katika uwanja wa Stamford Bridge ambao walicheza mechi moja mapema wiki hii.

Conte alisema: Ni ngumu kudhani kwamba ni bahati mbaya . Hii ni mara ya nne.

''Iwapo kuna mtu anataka kufanya mzaha nami, basi ajue kwamba mimi sio mtu wa kufanyia mzaha''.

Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 48 hivi majuzi alihoji ni kwa nini kikosi chake kililazimika kucheza dhidi ya Liverpool siku tatu baada ya kuelekea kucheza dhidi ya Qarabag ya Azerbaijan.

Pia amelalamika kuhusu mechi dhidi ya Manchester City na Watford ambazo Chelsea ilicheza baada ya mechi za klabu bingwa Ulaya.

Mada zinazohusiana