Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 02.12.2017

Mesut Ozil
Image caption Mesut Ozil

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anataka kumsajili kiungo wakati wa Arsenal na Ujerumani mwenye umri wa miaka 29 Mesut Ozil. (Telegraph)

Liverpool wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Brazil, 25, Philippe Coutinho kwa Barcelona mwezi Januari, lakini iwapo klabu hiyo itatoa dau la £127m. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Mshambuiaji wa Inter Milan raia wa Argentina Mauro Icardi, 24, ana thamani ya Yuro 200m kulingana na ajenti wa mchezaji huyo. (Corriere dello Sport, via BeInSport)

Haki miliki ya picha liverpool fc
Image caption Phillipe Countinho

Watford inamlenga mshambuliaji wa Leicester na Algeria mwenye umri wa miaka 29 Islam Slimani. (Watford Observer)

Real Madrid wamezuia usajili wa dau la £38m wa Vinicius Junior na wameamua kumuacha katika klabu yake ya Brazil ,Flamengo kwa msimu mwengine huku kinda huyo mwenye umri wa miaka 17 akitarajiwa kujiunga na klabu hiyo kwa mechi za maandalizi ya msimu ujao mwaka ujao (AS)

Tottenham imekataa kuongeza mishahara ya wachezaji wake licha ya hofu kwamba mazungumzo ya kuongeza kandarasi yamekwama kati ya timu hiyo na beki wa ubelgiji Toby Alderweireld. (Daily Mail)

Image caption Beki wa Ubelgiji Toby Alderweireld

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amechekeshwa na madai kwamba Barcelona imeweka bei ya kumnunua mshambuliaji wa Brazil Philippe Coutinho, 25, katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (ESPN)

Mkufunzi wa klabu ya Bournemouth Eddie Howe atafanya mazungumzo na mshambuliaji wa klabu hiyo Lewis Grabban, 29, ambaye yuko katika klabu ya Sunderland kwa mkopo (Bournemouth Echo)

Image caption Mchezaji wa Manchester United Paul Pogba

Paul Pogba, ambaye aliwagharimu Manchester United dau lililoweka rekodi ya £89m msimu uliopita wa 2016, anaamini kwamba kiungo wa kati wa Tottenham Dele Alli ana thamani ya zaidi ya £100m. (London Evening Standard)

Winga wa Leicester Riyad Mahrez anasema kuwa uwezekano wa yeye kujiunga na Arsenal msimu ujao uko asilimia 50. (Daily Mail)

Image caption Winga wa Leicester Riyad Mahrez

Kipa wa zamani wa Uingereza Gordon Banks alivaa tai ya timu ya Stoke City wakati aliposhiriki katika droo ya kombe la dunia nchini Urusi (Stoke Sentinel)

Beki wa Liverpool Joel Matip, 26, huenda akauguza jeraha la nyonga kwa hadi mwezi mmoja (Telegraph)

Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez anatarajia kwamba atapata makaribisho mema kutoka kwa mashabiki wa Chelsea wakati atakaporudi katika uwanja wa Stamford Bridge, ambapo alikuwa kaimu mkufunzi siku ya Jumamosi. (Daily Mail)

Mkufunzi wa Ubelgiji amesema kuwa familia yake itakuwa ikiunga mkono Uingereza wakati timu hizo mbili zitakapokutana katika kombe la dunia la mwaka ujao.(Mirror)

Mada zinazohusiana