Man United yaiadhibu Arsenal 3-1

Manchester United Waliiadhibu safu ya ulinzi ya Arsenal na kuwa timu ya kwanza kupata ushindi katika uwanja wa Emirates tangu mwezi Januari Haki miliki ya picha PA
Image caption Manchester United Waliiadhibu safu ya ulinzi ya Arsenal na kuwa timu ya kwanza kupata ushindi katika uwanja wa Emirates tangu mwezi Januari

Manchester United Waliiadhibu safu ya ulinzi ya Arsenal na kuwa timu ya kwanza kupata ushindi katika uwanja wa Emirates tangu mwezi Januari katika mojawapo ya mechi za ligi ya Uingereza msimu huu.

Kikosi cha Jose Mourinho kilipunguzwa na kuwa na wachezaji 10 katika dakika za mwisho baada ya Paul Pogba kupewa kadi nyekundu kwa kucheza visivyo na walisaidiwa na kipa wao David de Gea katika mechi yote.

Lakini licha ya hayo Arsenal iliadhibiwa mapema na Antonio Valencia wakati alipopata pasi mbaya ilioandaliwa na beki wa Arsenal Koscielny na kuweza kuiweka kifua mbele Manchester United kabla ya Jesse Lingard kufunga la pili baada ya kumpkoonya mpira Shkodran Mustafi.

Kabla ya Pogba kupewa kadi nyekundi alimshinda nguvu Koscielny na kumpatia pasi Lingaard ambaye alifunga bao la tatu na kuipatia United ushindi huo.

Mada zinazohusiana