Magolikipa wanaoshikilia rekodi pamoja na David de Gea

David de Gea Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption De Gea alisema tu kwamba: "Ilikuwa mechi nzuri kwangu"

Arsenal walishambulia lango la Manchester United mara 15 Jumamosi, lakini hawakufanikiwa kutikisa wavu isipookuwa mara moja tu - kikwazo chao David de Gea.

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho alisema uchezaji wa golikipa huyo wake ulikuwa "bora zaidi duniani".

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger pia alikiri kwamba Mhispania huyo alciheza kwa ustadi mkubwa na kwamba "alikuwa ndiye mchezaji bora wa mechi kwa mbali sana".

Uchezaji wake ulikuwa muhimu sana kwani uliwasaidia kulaza Arsenal 3-1 - na pia ulifikia rekodi Ligi ya Premia.

Hatua yake ya kuzima makombora 14 inamfanya kushikilia rekodi ya kuzuia makombora mengi zaidi mechi moja Ligi Kuu England pwa pamoja na mlindalango wa zamani wa Newcastle Tim Krul na kipa wa zamani wa Sunderland Vito Mannone.

Waliozuia makombora mengi zaidi mechi moja EPL tangu Agosti 2003 (Opta walipoanza kufuatilia data)

Tarehe Timu Mchezaji Mpinzani Aliokoa
19 Apr 2014 Sunderland Vito Mannone Chelsea 14
2 Des 2017 Man Utd David de Gea Arsenal 14
10 Nov 2013 Newcastle Tim Krul Tottenham 14
21 Mar 2015 West Brom Boaz Myhill Man City 13
7 Nov 2004 Fulham Mark Crossley Newcastle 13
2 Jan 2017 Sunderland Vito Mannone Liverpool 13
28 Feb 2016 Swansea Lukasz Fabianksi Tottenham 13
8 Apr 2006 Man City David James Tottenham 13

Nguzo ya Man City

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption De Bruyne aliondoka EPL mara ya kwanza alipoenda Wolfsburg awali kwa mkopo kutoka Chelsea 2012

Kevin de Bruyne, kiungo wa kati wa Manchester City mwenye miaka 26, alisaidia ufungaji wa bao mara ya nane msimu huu ligini.

Alisambaza mpira na kumuwezesha David Silva kufunga mechi ambayo walilaza West Ham 2-1.

Amesaidia ufungaji wa mabao 35 ligini akiwa an City tangu awachezee mechi ya kwanza Septemba 2015.

Hakuna mchezaji mwingine ligi tano kuu za Ulaya (England, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Uhispania) amesaidia ufungaji wa mabao mengi kama yeye. Amemwacha Mesut Ozil wa Arsenal kidogo.

Mchezaji Amesaidia kufunga mabao
Kevin de Bruyne (Man City) 35
Mesut Ozil (Arsenal) 32
Christian Eriksen (Tottenham) 30
Luis Suarez (Barcelona) 30
Neymar (Barcelona na PSG) 29
Lionel Messi (Barcelona) 29
Angel di Maria (PSG) 27

Mabao ya kujifunga

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Dunk alijifunga na kuwasaidia Liverpool kulaza klabu yake Brighton 5-1 Jumamosi

Jumamosi, beki wa Brighton Lewis Dunk alijifunga kwa mara ya tatu msimu huu, na kuwasaidia Liverpool kulaza timu yake 5-1.

Ina maana kwamba amejifunga kila mechi tano. Rekodi hata hivyo inashikiliwa na beki wa zamani wa Charlton Richard Rufus ambaye alijifunga mabao matano katika mechi 99.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rufus aliwafungia Charlton mabao sita Ligi ya Premia - hivyo angalau aliwafaa pia kwa mabao

Mabao ya kujifunga Ligi ya Premia (waliojifunga mabao matano na zaidi)

Mchezaji Mechi alizocheza Mabao ya kujifunga Mechi kwa kila bao la kujifunga
Richard Rufus 99 5 19.8
Michael Duberry 161 5 32.2
Martin Skrtel 242 7 34.5
Scott Dann 194 5 38.8
Neil Ruddock 195 5 39
Gareth McAuley 199 5 39.8
Richard Dunne 431 10 43.1
Frank Sinclair 288 6 48
Wes Brown 308 6 51.3
Henning Berg 275 5 55

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii