Liverpool, Monaco, Spurs zamaliza hatua ya makundi kwa ushindi

Liverpool Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Philippe Coutinho alifunga hatriki katika mchezo dhidi ya Spartak Moscow

Michezo nane ya mwisho ya hatua ya makundi ya klabu bingwa barani ulaya imechezwa usiku huu na hivyo kukamilisha jumla ya timu kumi sita zilizosonga mbele.

Majogoo wa Liverpool, wameibuka na ushindi wa kishindo nyumbani kwa kuichapa Spartak Moscow magoli 7-0 huku Maribor wakitoka sare ya 1-1 na Sevilla hivyo katika kundi E ni Liverpool na Sevilla zinasonga mbele.

Katika kundi F, Waholanzi wa Feyenoord wakaifunga Napoli 2 - 1,nao Shakhtar Donetsk wakapata ushindi muhimu wa mabao 2 - 1 dhidi ya Manchester City hivyo Man City na Shakhtar Donetsk wanasonga mbele katika hatua ya kumi na sita bora.

Wareno wa Fc Porto wakatakata nyumbani kwa ushindi wa goli 5-2 dhidi ya Wafaransa wa Monaco nao Wahuni wa Besiktas wakashinda ugenini kwa ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Leipzig. hivyo katika kundi G,Fc Porto na Besiktas ndio wanafuzu kwa hatua ya kumi na sita bora.

Katika kundi H, Real Madrid na Tottenham zimefuzu kusonga mbele baada ya Real Madrid kuwachapa Borussia Dortmund 3-2, Huku Tottenham Hotspur wakishinda 3 - 0 dhidi ya APOEL Nicosia.