Hull City yamteua Nigel Adkins kuwa meneja wao mpya

Nigel Adkins
Image caption Nigel Adkins

Klabu ya Hull City ya Uingereza imemteua meneja wa zamani wa Southampton na Reading Nigel Adkins kuwa mkufunzi wao mkuu kwa mkataba wa miezi 18.

Adkins, 52, anachukua nafasi ya Mrusi Leonid Slutsky aliyeiaga timu hiyo siku ya Jumapili, klabu hiyo ikiwa katika nafasi ya 20 katika ligi ya Championship.

Adkins ambaye hakuwa kazini tangu kufutwa kwake na Sheffield United mwezi Mei 2016, aliwasaidia watakatifu hao wa St Marys kupanda ngazi hadi kwenye Ligi ya Premia mwaka 2012.

Meneja huo ataongoza mazoezi siku ya Alhamisi na mechi yake ya kwanza kuwaongoza itakuwa ugenini Brenford siku ya Jumamosi.

Adkins alikuwa mlinda lango wa zamani wa Tranmere Rovers F.C. na Wigan na alihamia Southampton mwezi Septemba mwaka 2010.

Baada ya kuwaongoza Southampton na kupanda ngazi ya kushiriki ligi ya Premia, alifutwa mwezi Januari mwaka 2013 huku Mauricio Pochettino akichukua nafasi yake.

Majukumu yake ya umeneja mara mbili hayajafanikiwa, kwa Reading FC na Sheffield United.

Mada zinazohusiana