Wilshere na Walcott wanataka Wenger ajikune kichwa Arsenal

Jack Wilshere Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jack Wilshere

Jack Wilshere na Theo Walcott wanatumai kwamba meneja wa Arsenal Arsene Wenger atafurahishwa kiasi cha kuwatumia kwenye mechi baada yao kucheza vyema sana Alhamisi.

Walciheza vizuri sana mechi ya Europa League ambayo walishinda kwa mabao mengi dhidi ya Bate Borisov.

Wawili hao hawajapewa nafasi ya kucheza kikosi cha kuanza mechi Arsenal katika Ligi ya Premia msimu huu, lakini wote wawili walitikisa wavu na kusaidia Arsenal kulaza Bate Borisov 6-0 na kumaliza mechi za Kundi H kwa ushindi.

"Kuna ushindani mkali unapokuwa unachezea Arsenal. Tufanya kadiri ya uwezo wetu kumfanya meneja ajikune kichwa akijaribu kuchagua wachezaji wa kutumia," Walcott amesema.

Wilshere, aliyefunga bao lake la kwanza tangu Mei 2015 aliongeza, "Jambo tunaloweza kufanya tunapopewa fursa na kumfanya meneja ajikune kichwa."

Arsenal walijiweka kifua mbele kupitia Mathieu Debuchy, kisha Walcott akafunga akifuatiwa na Wilshere.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jack Wilshere amechezeshwa kama nguvu mpya Arenal mara nne Ligi ya Premia msimu huu

Beki wa Bate Denis Polyakov alijifunga kutokana kwa krosi ya Walcott kipindi cha pili kabla ya Olivier Giroud kufunga mkwaju wa penalti baada ya Nemanja Milunovic kumwangusha Walcott.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Theo Walcott alifunga bao lake la nne msimu huu dhidi ya Bate Borisov

Mohamed Elneny aliongeza la sita baada ya kupokea mpira kutoka kwa a Wilshere.

Baada ya Arsenal kulazwa 3-1 na Manchester United nyumbani wikendi, ilikuwa fursa kwa baadhi ya wachezaji waliowekwa pembeni kung'aa.

Wenger alifanya mabadiliko 11 kwenye kikosi chake kilicholazwa na United kwa mechi hiyo ya Alhamisi.

Mada zinazohusiana