Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 10.12.2017

Jose Mourinho Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jose Mourinho

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anajiandaa kulipa pauni milioni 95 kumsaini mchezaji wa safu ya kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic. (Sunday Express)

Real Madrid watampa ofa kipa wa Tottenham na Ufaransa Hugo Lloris, 30, ikiwa Tottenham itashindwa kupata kombe msimu huu. (Sunday Mirror)

Arsenal itatoa ofa msimu ujao kumsani winga wa Paris St-Germain mreno Goncalo Guedes, 21. (Mail on Sunday)

Haki miliki ya picha PA
Image caption Eden Hazard

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 26, anasema kuwa hana haraka ya kuondoka klabu hiyo, baada ya raia huyo wa Ubelgjji kuhusishwa na kuhama kwenda Real Madrid. (Onze Mondial, via Sun on Sunday)

Kipa wa Chelsea Thibaut Courtois amesema hakuna sababu ya yeye kukosa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. Mchezaji wa umri wa miaka 25 anahusishwa na kuhamia Uhispania. (VTM Stadion, via Evening Standard)

Mchezaji wa safu ya kati wa Liverpool Philippe Coutinho anataka hakikisho kuwa ataruhusiwa kujiunga na Barcelona msimu ujao. (Sunday Mirror)

Chelsea watamruhusu mshambuliaji raia wa Ubelgiji Michy Batshuayi, 24, kuondoka kwa mkopo mwezi Januari. (Sun on Sunday)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Philippe Coutinho

Kipa wa England na Manchester City Joe Hart, 30, hataruhiswa kumaliza mkopo wake huko Westham mwezi Januari. (Sunday Times - subscription required)

Liverpool, Manchester United na Tottenham wamejiunga na Everton katika kumasaini mlinzi wa Augsburg ya Ujerumani Philipp Max, 24. (Mail on Sunday)

Everton na Westham wanamtazama mshambulioaji wa Leicester Josh Eppiah, 19. (ESPN)

Manchester United wamemualika winga raia wa Canada Alphonso Davies, anayeichezea Vancouver Whitecaps, kufanya mazoezi nao. (CTV, via Sunday Express)

Mada zinazohusiana