Southampton 1-1 Arsenal

Olivier Giroud Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Olivier Giroud

Olivier Giroud alisaidia Arsenal kujiapati pointi baada ya kuwafungia kwa kichwa licha ya Arsenal kuonekana kulemewa na Southampton.

Mshambuliaji huyo mfaransa aliitumia vizuri krosi kutoka kwa Alexis Sanchez dakika ya 88.

Kulikuwa na dalili kuwa kasi ya chini ya Arsenal ingawanyima mafinikio ya wiekendi wakati Charlie Austin aliwafungia Southampton dakika tatu baada ya kuanza kwa mechi.

Southampton tena ikakosa nafasi muda mfupi baada ya bao la kwanza wakati Petr Cech alisukuma mkwaju uliopanguliwa na kipa na kisha kugonga mwamba wa goli.

Sare inawapeleka mbele Arsenal kwa pointi lakini bado wako nyuma kwa mabao ya nambari nne Liverpool.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Southampton 1-1 Arsenal

Mada zinazohusiana