Man United yalala 2-1 kwa Man City

City haijafungwa mchezo wowote kwenye ligi msimu huu
Image caption City haijafungwa mchezo wowote kwenye ligi msimu huu

Manchester City imeendeleza ubabe wake kwenye ligi kuu soka ya England baada ya kumchapa hasimu wake wa jiji moja Manchester United 2-1.

Katika mchezo huo ambao City ilimiliki mpira wakati mwingi, ilipata goli lake la kwanza kupitia David Silva dakika ya 43 kabla ya Marcus Rashford kusawazisha dakika ya 45 na Nicolás Otamendi kupachika la pili na la ushindi dakika ya 54.

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema kwa sasa ni wazi asilimia kuwa ya ubingwa msimu huu ikaenda kwa City.

Image caption Nusura Lukaku asawazishe matokeo dakika za mwisho wa mchezo kabla ya mlinda mlango wa City Ederson kuokoa

''Wamecheza vizuri, wengi walitarajia hili, ni vigumu kuwakabili kama hauna timu imara zaidi yao, tumemkosa Pogba ambaye angeweza kuleta madhara kwao, nafikiri wanaweza kuwa mabingwa msimu huu,'' alisema Mourinho.

Meneja wa City Pep Guardiola ameisifu timu yake kwa kucheza kama Barcelona na kuongeza kuwa vile alivyotoa maelekezo ndivyo walivyofanya.

City ambao wamepoteza alama mbili tu katika michezo 16 wanasalia kileleni wakiwa na alama 46 , huku United ikiwa na alama 35.