Mourinho arushiwa maji na maziwa kufuatia kushindwa kwa Man U

Manchester City players celebrate after their Derby win at Manchester United Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manchester City walisherehekea mbele ya mashabiki

Maneja wa Manchester United Jose Mourinho amerushiwa maji na maziwa kufuati kushindwa na Manchester City huko Old Trafford.

United walikasirika kutokana na kile walichokiona kuwa kusherehekea kupindukia kwa City kufuati ushindi wa Jumapili wa bao 2-1 ambalo lilifungua mwaka wa pointi 11 kileleni.

Wachezaji wa City walisherehekea na mashabiki wao baada ya kipenga cha mwisho na maafisa wengine wakajaribu kumshawishi meneja Pep Guardiola kujiunga nao lakini akakataa.

Baada ya wachazaji kuondoka uwanjani inaeleweka kuwa Mourinho alilalamika akiwa ndani ya chumba cha kubadilishia nguo kabla ya kurudi kwa mahojiano.

Upande wa City ulijibu huku kipa wa Brazil Ederson akijibizana na Mourinho kwa lugha ya kireno.

Haki miliki ya picha Leroy Sane, Twitter
Image caption Wachezaji wa City wakishrrehekea Old Trafford

Mada zinazohusiana