Chelsea wapewa Barcelona Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya

Fabregas & Messi Haki miliki ya picha Getty Images

Chelsea wamepangwa kukutana na Barcelona hatua ya 16 bora katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, Tottenham nao wakapewa mabingwa wa Italia Juventus baada ya droo kufanywa.

Viongozi wa Ligi ya Premia Manchester City watakutana na FC Basel ya Uswizi, Manchester United wakutana na Sevilla wanaocheza La Liga nao Liverpool wakutane na FC Porto ya Ureno.

Mabingwa watetezi Real Madrid watakutana na Paris St-Germain.

Klabu tano kutoka England zilifuzu kwa hatua ya makundi msimu huu, ambayo ni rekodi.

Chelsea ndio pekee wa Uingereza waliofuzu wakiwa wa pili kutoka kundi lao, klabu nyingine zote zilimaliza kileleni.

Washindi wa makundi watakuwa ugenini mechi za kwanza 13/14 na 20/21 Februari na nyumbani mechi za marudiano mbamo 6/7 na 13/14 Machi.

Fainali itachezewa Kiev mnamo 26 Mei.

Droo kamili: Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya

Juventus v Tottenham

FC Basel v Manchester City

Porto v Liverpool

Sevilla v Manchester United

Real Madrid v PSG

Shakhtar Donetsk v Roma

Chelsea v Barcelona

Bayern Munich v Beskitas

Mada zinazohusiana