Europa League: Arsenal wakabidhiwa Ostersunds, Celtic wapewa Zenit St Petersburg

Mesut Ozil Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsenal hawajawahi kushindwa na klabu ya Sweden mashindano ya Ulaya

Celtic wamepangwa kucheza dhidi ya Zenit St Petersburg hatua ya 32 bora ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League, nao Arsenal wakapewa FK Ostersunds ya Sweden.

Celtic, waliomaliza wa tatu kundi lao la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na wakashushwa daraja hadi Europa League, watacheza dhidi ya klabu hiyo ya Urusi mnamo 15 Februari.

Arsenal, walimaliza kileleni kundi lao Europa League, na watasafiri Sweden kwanza.

Mechi za marudiano zitachezwa 22 Februari.

Zenit, waliowalaza Rangers fainali ya michuano hiyo ilipokuwa inafahamika kama Kombe la Uefa mwaka 2008, wako chini ya meneja wa zamani wa Manchester City Roberto Mancini.

Klabu ya FK Ostersunds ambayo mkufunzi wake ni Mwingereza beki wa zamani wa Southampton Graham Potter ilianzishwa Oktoba 1996, wakati Arsene Wenger alipokuwa anaanza kazi ya umeneja Arsenal.

Arsenal hawajawahi kushindwa Ulaya na klabu ya Sweden - wameshinda tatu na kutoka sare moja.

Fainali itachezewa Parc Olympique Lyonnais mnamo 16 Mei.

Droo ya 32 bora Europa League

Borussia Dortmund v Atalanta

Nice v Lokomotiv Moscow

FC Copenhagen v Atletico Madrid

Spartak Moscow v Athletic Bilbao

AEK Athens v Dynamo Kiev

Celtic v Zenit St Petersburg

Napoli v RB Leipzig

Red Star Belgrade v CSKA Moscow

Lyon v Villarreal

Real Sociedad v Red Bull Salzburg

Partizan Belgrade v Viktoria Plzen

Steaua Bucharest v Lazio

Ludogorets v AC Milan

Astana v Sporting Lisbon

FK Ostersunds v Arsenal

Marseille v Braga

Mada zinazohusiana