Hemed: Wachezaji wa Zanzibar katika Cecafa hawana doa
Huwezi kusikiliza tena

Hemed: Wachezaji wa Zanzibar katika Cecafa hawana doa

Timu ya taifa ya kandanda ya Zanzibar wiki hii imegonga vichwa vya habari hasa kwenye mitandao ya kijamii kwa madai ya kutumia dawa za kuongeza nguvu baada ya baadhi ya wachezaji wa timu hiyo, kupimwa katika mashindano ya kombe la Cecafa ya Senior Challenge yanayofanyika nchini Kenya.

Zanzibar imefanya vyema kinyume na matarajio ya wengi mpaka ikashinda Tanzania Bara (Tanganyika) na kufuzu kwenye nusu fainali ambapo kesho itapambana na Uganda mjini Kisumu.

John Nene yuko huko na leo hii amezungumza na kocha wa Zanzibar Suleiman Hemed ambaye amekanusha madai hayo.

Mada zinazohusiana