Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 15.12.2017

Renato Sanches

Chanzo cha picha, Rex Features

Manchester United wameulizia kumhusu kiungo wa kati wa Chelsea na Brazil Willian, 29. (Daily Mail)

Meneja wa United Jose Mourinho pia yuko tayari kumuuza kiungo wa kati wa Armenia Henrikh Mkhitaryan, 28, majira ya joto na anataka kumnunua kiungo wa Arsenal na Ujerumani Mesut Ozil, 29, kujaza nafasi yake. (Daily Mirror)

Chelsea nao huenda wakamtumia mshambuliaji wa Belgium Michy Batshuayi, 24, kama kikolezo kwenye mkataba wa kumchukua winga wa Monaco na Ufaransa Thomas Lemar, 22, ambaye amekuwa pia akitafutwa na Liverpool na Arsenal.(Sun)

Kiungo wa kati wa Bayern Munich na Ureno Renato Sanches, 20, huenda akarejea kwa klabu yake mapema kutoka kwa mkopo Swansea Januari. (Mais Futebol)

Chanzo cha picha, Getty Images

Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone naye amemhakikishia mshabuliaji Mfaransa Antoine Griezmann kwamba hatimaye ataruhusiwa kuihama klabu hiyo ya La Liga. (Daily Mail kupitia L'Equipe)

Liverpool bado wana hamu ya kumnunua mkabaji wa Southampton mwenye umri wa miaka 26 kutoka Uholanzi Virgil van Dijk mwezi Januari. (Liverpool Echo)

Hata hivyo, Manchester City wanataka kumuongeza beki wa kati kwenye kikosi chao Januari na huenda pia wakawasilisha ombi la kutaka kumnunua Van Dijk, ingawa viongozi hao wa Ligi ya Premia pia wanataka kumnunua mchezaji wa Real Sociedad Inigo Martinez, 26. (Goal)

Meneja wa City Pep Guardiola pia atarudi sokoni kumtafuta beki wa kushoto mwezi Januari. (Manchester Evening News)

Meneja wa Everton Sam Allardyce amesema hatapinga iwapo klabu hiyo itaamua kumuuza Ross Barkley, 24, Januari. Kiungo huyo wa kati wa England bado hajatia saini mkataba mpya. (Daily Mirror)

Barcelona wanataka kumnunua beki wa Manchester United kutoka Uholanzi Daley Blind, 27, bila ada yoyote mkataba wake utakapofikia kikomo majira ya joto. (Marca)

Manchester United watashindana na Juventus katika kutaka saini ya mchezaji wa Monaco na Brazil Fabinho, 24. (Tuttosport, kupitia Talksport)

Wawakilishi kutoka klabu ya Uturuki Fenerbahce wanasafiri Liverpool katika juhudi za kutaka kumchukua kwa mkopo mchezaji wa Serbia Marko Grujic, 21. (Takvim, kupitia Talksport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Lemar aliwasaidia Monaco kushinda Ligue 1 msimu uliopita

Kiungo wa kati wa England Jack Wilshere, 25, naye amethibitisha kwamba bado anasubiri kufahamishwa na Arsenal ni lini mazungumzo kuhusu mkataba wake yataanza. (Telegraph)

Aston Villa nao wanataka kumchukua mshambuliaji wa Burnley na Bermuda Nakhi Wells mwezi ujao. (Birmingham Mail)

Meneja wa Paris St-Germain Unai Emery naye nyumba yake imeporwa, na wezi wakaondoka na jezi mbili za Neymar pamoja na nyaraka kuhusu uhamisho na ununuzi wa wachezaji za PSG. (Le Point)

John Hartson anaamini kwamba Jose Mourinho mwenyewe hawezi kutatua shinda za klabu ya Rangers na anaamini kwamba bodi ya klabu hiyo yenye makao yake Glasgow ndiyo tatizo. (Daily Record)

Mkufunzi mkuu wa Crystal Palace Roy Hodgson amemuonya mshambuliaji wake ambaye amekuwa butu siku hizi Christian Benteke kwamba hawezi kuwa na mashabiki kwenye timu, Palace wanapojaribu kupanda kwenye jedwali. (Daily Mail)

Tottenham lazima wajidhihirishe kwamba ni timu inayojitosheleza bila 'Harry Kane' kwa mujibu wa mchezaji wao mmoja Harry Winks. (Daily Mail)

Chanzo cha picha, Paul Pogba/Instagram

Maelezo ya picha,

Paul Pogba has revealed his new flame-coloured hairstyle to the world. His caption was 'Hair is burning'.

Everton walimjumlisha Lil Wayne kwenye ujumbe wao wa Twitter badala ya Wayne Rooney baada ya ushindi wao 1-0 ugenini Newcastle. (BBC Sport)

Kiungo wake wa Manchester United Paul Pogba naye amepiga picha na kuipakia kwenye Twitter kuonesha mtindo wake mpya. (Twitter).