Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 16.12.2017

Carlo Ancelotti Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Carlo Ancelotti ameshinda mataji ya ligi katika nchi nne, na ni meneja mwenza mwenye ufanisi mkubwa katika historia ya kombe la Ulaya

Carlo Ancelotti atarudi Stamford Bridge na kuwa meneja wa Chelsea kabla ya kuanza kwa msimu mpya. (Daily Record)

Winga wa Monaco Thomas Lemar, 22, anawindwa na Chelsea, wanaotayarisha makubaliano ya fedha na mchezaji ya mshambuliaji Michy Batshuayi. (Daily Mirror)

Batshuayi, 24, anatarajia kuondoka Chelsea mwezi ujao kwa mkopo kupunguza hofu ya kupoteza nafasi yake katika kikosi cha Ubelgiji kitakachocheza katika kombe la dunia. (London Evening Standard)

Mchezaji kiungo cha kati raia wa Armenia Henrikh Mkhitaryan, 28, ametemwa na mkufunzi wa Manchester United, Jose Mourinho baada ya kuzuka mzozo kati yao wakati wa tathmini ya mechi katika uwanja wa mazoezi mwezi uliopita. (ESPN)

Mkufunzi huo wa ManUnited boss Mourinho ana nafasi ya kusajili wachezaji mwezi ujao, licha ya kwamba sio shabiki wa msimu wa usajili Januari. (Daily Mail)

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane anasemamchezaji kiungo cha mbele wa Liverpool Mohamed Salah "ni mchazaji nnaye mpima kiwango sana" kufuatia kocha wa mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Misri Hector Cuper, kusema kuwa klabu hiyo ya Uhispania itamnunua mchezaji huyo wa miaka 25. (Sun)

Arsenal itafanya mazungumzo ya kandarasi na mchezajiw a kiungo cha kati mwenye umri wa miaka 25 Jack Wilshere kabla ya mwisho wa mwezi. (London Evening Standard)

Huenda Gunners ikapoteza wachezaji watatu msimu ujao wa joyo wakati bosi Arsene Wenger anapojitayarisha kwa mabadiliko yake makubwa. (Daily Mirror)

Liverpool na Tottenham zimeonywa kuwa winga wa Fiorentina Federico Chiesa atawagharimu kiasi cha £53m. (La Stampa, via Talksport)

Kwengineko...

Tizama sura mpya ya Didier Drogba...

Haki miliki ya picha Twitter @didierdrogba

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola anasema "kamwe" hawaambii wachezaji wake wacheze fauli, kauli aliyomjibu kocha mpinzani wake wa Manchester United, Jose Mourinho aliyesema kuwa upande wake unacheza "fauli za kupangwa". (Guardian)

Guardiola anasema beki wa kulia wa Manchester City Kyle Walker, 27, ni "mojawapo ya walio bora duniani" katika nafasi yake hivi sasa lakini ananuia kumfanya mchezaji huo wa timu ya kimataifa ya England kuwa bora zaidi. (Daily Express)

Sturridge asaidia Liverpool kulaza Spurs

Mwamba wa soka Argentina Diego Maradona anasema ameiambia Real Madrid imsajili Kylian Mbappe, 18, kabla ya Paris St-Germain imwahi, lakini Los Blancos alikataa kwasababu ya Cristiano Ronaldo. (AS, via Goal)

Mchezaji kiungo cha kati wa Tottenham Mousa Dembele amegundua mali iliyopotea yenye thamani ya £1m katika dari la nyumba yenye miaka 700 huko Antwerp. (London Evening Standard)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii