Pep Guardiola kuzungumza na Manchester City kuhusu mkataba

Pep Guardiola Haki miliki ya picha Getty Images

Manchester City watafanya mazungumzo na meneja wao Pep Guardiola kuhusu mkataba mpya majira yajayo ya joto huku wakiendeleza lengo lao la kuunda himaya ya soka itakayotishia ile ya Manchester United.

United walishinda mataji yao manane kati ya jumla ya 11 Ligi ya Premia wakiwa chini ya meneja wao wa Sir Alex Ferguson.

City wanataka kuiga ubabe kama huo.

Walilaza Tottenham 4-1 Jumamosi na kuendeleza mkimbio wao wa kushinda mechi mfululizo ligini hadi 16, na kusalia alama 11 mbele ya United kileleni.

Mkataba wa Guardiola wa sasa utamalizika 2019.

Guardiola, ambaye awali alikuwa mkufunzi Barcelona na Bayern Munich, aliteuliwa meneja wa City majira ya joto2016.

Msimu wa kwanza walimaliza wa tatu Ligi ya Premia lakini klabu hiyo iliendelea kuwa na imani naye.

Mada zinazohusiana