Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 19.12.2017

Haki miliki ya picha Empics
Image caption David Luiz

Manchester City wako tayari kujiunga na Arsenal na Chelsea Arsenal wana mpango wa kumsaini mlinzi wa Chelsea David Luiz, 30. (Daily Express)kumatafua wing'a wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 25. (Daily Mirror)

Arsenal wanaweza kutoa ofa ya pauni milioni 25 kwa mBrazil huyo mwezi Januari. (Sun)

Real Madrid wako kwenye mazungumzo na mchezaji wa Chelsea Eden Hazard, 26.

Mchezaji wa safu ya kati wa Real Madrid Marco Asensio, 21, amekiambia klabu hiyo kuwa ataondoka ikiwa Hazard atajiunga nacho (Diario Gol,kupitia Daily Star)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Antoine Griezmann

Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, 26, anatarajiwa kujiunga na Barcelona (BBC Radio 5 live

Manchester United inataka zaidi ya pauni milioni 35 kwa mchezaji huyo wa safu ya kati wa miaka 28 Henrikh Mkhitaryan. (Daily Mail)

Mchezaji aliyekuwa akiwindwa na Machester United Sergej Milinkovic, 22, anasema yuko na furaha huko Lazio na kuzima jitihada za Mourinho za pauni milioni 95 kumsaini mchezaji huyo wa safu ya kati. (Mediaset Premium, kupitia Daily Star)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema kuwa hatawaruhusu Manchester City kumsaini mlinzi Virgil van Dijk, 26, kutoka Southampton. (Goal)

Meneja wa Southampton Mauricio Pellegrino ataiambia bodi ya klabu yake kuwa watakataa ofa yoyote ya kununuliwa Van Dijk mwezi Jauaria. (Daily Echo)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Virgil van Dijk

Mada zinazohusiana