Tetesi za soka Ulaya Jumatano 20.12.2017

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anapanga kutoa rekodi ya dau la Uingereza la £90m kumnunua mchezaji wa Chelsea na Ubelgiji ,26, Eden Hazard. (Sun)
Image caption Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anapanga kutoa rekodi ya dau la Uingereza la £90m kumnunua mchezaji wa Chelsea na Ubelgiji ,26, Eden Hazard. (Sun)

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anapanga kutoa rekodi ya dau la Uingereza la £90m kumnunua mchezaji wa Chelsea na Ubelgiji ,26, Eden Hazard. (Sun)

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright ameitaka klabu ya Manchester City kumnunua mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah. (Sky Sports via the Daily Express)

Mkufunzi wa Everton Sam Allardyce anataka kumpatia mshambuliaji wa Uingereza na Arsenal Theo Walcott, 28, njia ya kuondoka Arsenal mbali na kumyakua kiungo wa kati wa Sevilla na Ufaransa Steven N'Zonzi, 29. (Daily Mirror)

Newcastle United imejiunga katika harakati za kumsajili beki wa Chelsea David Luiz katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari , lakini inataka kumchukua mchezaji huyo wa Brazil kwa mkopo (Shields Gazette)

Atletico Madrid wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 26, kwenda Manchester United baada ya kuiripoti Barcelona kwa Fifa kuhusu madai ya klabu hiyo ya kutaka saini ya mchezaji huyo kinyume na sheria. (Daily Mirror)

Leicester City inajiandaa kumsajili beki wa Ureno na Benfica Andre Almeida, 27. (Leicester Mercury)

Mshambuliaji wa Liverpool na Wales Ben Woodburn, 18, ataruhusiwa kuondoka kwa mkopo mwezi Januari ili kuweza kupata nafasi ya kucheza. (Daily Mail)

Brighton wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Spartak Moscow na Cape Verde Ze Luis, 26. (Sun)

Klabu ya China ya Chongqing Dangdai Lifan haina haja ya kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona Andreas Iniesta kwa kuwa wanaamini kwamba sio mzuri sana kucheza katika ligi ya Uchina ya Super League (Marca via the Chongqing Morning Post)

Real Madrid inajiandaa kumlipa kipa wa Athletic Bilbao na Uhispania Kepa Arrizabalaga's Yuro milioni 20 mwezi Januari na kuthibitisha usajili wake katika wiki ya kwanza ya mwaka mpya.. (AS)

Beki wa Barcelona Javier Mascherano, 33, anakaribia kujiunga na klabu ya China ya Hebei Fortune. (Sport)

Mkufunzi wa Aston Villa Steve Bruce ana hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Burnley na Bermuda Nahki Wells, 27, na mshambuliaji wa Leicester na Argentina Leonardo Ulloa, 31. (Birmingham Mail)

Mkufunzi wa Stoke Mark Hughes anaendelea kuungwa mkono na bodi ya klabu hiyo kabla ya mechi ya Jumamosi dhidi ya West Brom licha ya klabu hiyo kuwa pointi moja juu ya eneo la kushushwa daraja. (Sky Sports)

Mwenyekiti wa Stoke Peter Coates anasema kuwa kutakuwa na fedha za kutumia katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari licha ya kwamba haijulikani ni nani atakayekuwa mkufunzi.(Stoke Sentinel)

Aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Mikel Arteta ameorodheshwa miongoni mwa wakufunzi wa siku zijazo wa Arsenal huku klabu hiyo ikiendelea na mipango ya mkufunzi atakayemrithi Wenger baada ya kuondoka kwake. (Telegraph)

Winga wa Wales na Liverpool Harry Wilson, 20, amekataa kusaini kandarasi mpya katika klabu hiyo ya Anfield. (ESPN)

Mkufunzi wa West Ham David Moyes anataka klabu hiyo kuwanunua viungo wa kati katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari baada ya kuwashirikisha kinda Declan Rice na Domingos Quina katika kombe la Carabao dhidi ya Arsenal. (the42.ie)

Manchester City inapigiwa upato kushinda mataji manne baada ya kufika nusu fainali ya kombe la Carabao , lakini meneja wa klabu hiyo anasema haiwezekani.(Telegraph)

Mashabiki wa Manchester United huenda wakalazimika kulipa hadi £133 kwa tiketi za kombe la vilabu bingwa ugenini dhidi ya Sevilla. (Manchester Evening News)

Manchester United, Real Madrid, Juventus na Bayern Munich wamezindua jezi mpya lakini katika mchezo wa kompyuta wa Fifa wa wachezaji wa miaka 18.(Daily Mail)

Akaunti ya Twitter ya klabu ya Manchester City nchini Ufaransa imedai kuwa kiungi wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini sio mchezaji wa soka(Metro)

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anatarajiwa kujenga hospitali ya watoto nchini Chiole 2020. (Four Four Two) lakini ripoti nyengine zinasema kuwa hana mipango ya kujenga hospitali yoyote. (efe)

Mada zinazohusiana