Tomas Rosicky astaafu soka ya kulipwa

Mchezaji wa zamani wa Arsenal na taifa la Czech Tomas Rosicky amestaafu soka ya kulipwa Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mchezaji wa zamani wa Arsenal na taifa la Czech Tomas Rosicky amestaafu soka ya kulipwa

Mchezaji wa zamani wa Arsenal na taifa la Czech Tomas Rosicky amestaafu soka ya kulipwa.

Rosicky alijishindia mataji mawili ya kombe la FA na kuichezea Gunners kwa kipindi cha muda wa miaka 10 kutoka Borussia Dortmund 2006.

Raia huyo ambaye alianza soka yake ya kulipwa katika klabu ya Sparta Prague anasema kuwa majeraha yamemlazimu kustaafu.

''Siweze tena kuandaa mwili wangu kwa kiwango cha soka ya kulipwa'', mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 aliambia mtandao wa klabu ya Sparta.

''Mwili wangu ulikuwa ukiniambia kwa muda mrefu kwamba umechoka'', aliongezea Rosicky.

Mada zinazohusiana