Mwimbaji mashuhuri wa Korea Kusini Kim Jong-hyun kuzikwa leo

Kim Jong-hyun alikua mwanamuziki mashuhuri Korea Kusini
Image caption Kim Jong-hyun alikua mwanamuziki mashuhuri Korea Kusini

Mazishi ya mwimbaji mashuhuri wa Korea Kusini Kim Jong-hyun, yanafanyika leo hii mjini Seoul.

Mwanamuziki huyo ambaye pia alikua mtangazaji wa radio, mwandishi wa vitabu na mtunzi wa nyimbo, alipatikana amefariki katika tukio linalotajwa kuwa la kujiua.

Umati mkubwa wa watu umekusanyika kumsindikiza katika safari yake ya mwisho, huku mwili wake ukibebwa na gari aina ya limousine nyeusi kutoka hospitalini alipohifadhiwa kwa takriban siku tatu.

Image caption Picha yake iliwekwa hospital mjini Seoul

Ibada ya kumuaga kifamilia ilifanyika mapema pia mjini Seoul.

Mwanamuziki huyo aliyekua na miaka 27 akiimbia bendi ya Shinee, alipatikana ameanguka kutoka ghorofa moja ndefu siku ya Jumatatu.