''Wachezaji wa Bristol hawakujuwa wacheke au walie kwa kuilaza Man United ''

Mkufunzi wa Bristol akimkumbatia ball boy baada ya timu yake kuilaza Manchester United katika robo fainali ya kombe la Carabao. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkufunzi wa Bristol akimkumbatia ball boy baada ya timu yake kuilaza Manchester United katika robo fainali ya kombe la Carabao.

Wachezaji wa Bristol City hawakujua iwapo walifaa kucheka , kulia ama kukumbatiana baada ya kuilaza Manchester United katika robo fainali ya kombe la Carabao.

Klabu hiyo ya ligi ya daraja la kwanza nchini Uingereza ilipata ushindi wa 2-1 katika uwanja wa nyumbani wa Ashton Gate na hivyobasi kufika nusu fainali dhidi ya Manchester City.

Bao la dakika ya 93 la Korey Smith ndilo lililobainisha tofauti kati ya timu bizo mbili tangu 1980.

''Sikuamini. Tunahitaji usiku mwengine kama huu'', mkufunzi wa klabu hiyo Lee Johnson aliambia BBC Sport.

''Huku kukiwa na kelele katika uwanja, vijana walijawa na hisia, hawakujuwa walie,wacheke ama wakumbatiane''.

Johnson alikimbia kandokando ya mstari wa uwanja huo kusherehekea bao hilo la Smith, ambapo alimshika na kumkumbatia mvulana anayetumiwa kurusha mipira ndani ya uwanja huku kukiwa na visa vya furaha katika uwanja huo.

Haki miliki ya picha Empics
Image caption Bao la kwanza la Bristol dhidi ya Man United

''Sikujua la kufanya'',Johnson aliongezea. ''Nilitaka kukimbia na kusherehekea na vijana wangu lakini sikuweza kufanya hivyo''.

''Ball Boy ndiye alikuwa karibu nami.Ilikuwa furaha kumuona kwasababu nilitaka kusherehekea na mtu na ilibidi awe kijana huyo''.

Mada zinazohusiana