Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 21.12.2017

Swansea inajaribu kumrai mkufunzi wa zamani wa Man United Louis van Gaal kuwa meneja wake mpya
Image caption Swansea inajaribu kumrai mkufunzi wa zamani wa Man United Louis van Gaal kuwa meneja wake mpya

Swansea inajaribu kumrai mkufunzi wa zamani wa Man United Louis van Gaal kuwa meneja wake mpya baada ya kumfuta kazi Paul Clement. (Daily Mirror)

Mkufunzi wa zamani wa Stoke, West Brom na Crystal Palace Tony Pulis ni miongoni mwa wakufunzi wanaotarajiwa kumrithi Clement. (Daily Star)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 29, anakaribia kuhamia Paris St-Germain baada ya ajenti wake kuelekea katika mji mkuu wa Ufaransa kwa mazungumzo(Canal Plus - via Metro)

PSG itajaribu kumsajili Sanchez kwa dau la £25m ijapokuwa Manchester City bado wanamtaka mchezaji huyo wa Chile baada ya kushindwa kumpata mchezaji huyo kwa dau la £60m katika dirisha la uhamisho lililiopita. (Express)

Sanchez atasalia Arsenal mwisho wa msimu na baadaye ajiunge na Manchester City katika uhamisho wa bure , mpango ambao utampatia kipato cha £400,000 kwa wiki. (Daily Mirror)

Barcelona iko tayari kulipa £132m ili kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Sport - via Daily Mail)

Bale ameichezea Real Madrid mara 12 pekee msimu huu na kufunga mabao manne.Je Jumamosi ijayo itakuwa mechi yake ya mwisho ya El Classico ?

Atletico Madrid inasema kuwa beki Sime Vrsaljko, 25, anayelengwa na Liverpool, hataondoka mwezi ujao.. (Corriere dello Sport - via Daily Mirror)

Chelsea huenda wakagonga mwamba kumsajili winga wa Bayer Leverkusen Leon Bailey, 20, mwezi ujao lakini bado wanamtaka kiungo wa kati wa Everton Ross Barkley, 24, na mshambuliaji wa Monaco Thomas Lemar, 22. (London Evening Standard)

Lemar anadaiwa kutaka kuhamia Liverpool badala ya kwenda Stamford Bridge ama Arsenal. (Independent)

Arsenal na Liverpool wako katika mazungumzo ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos, 21. (Diario Gol - via Daily Star)

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa asilimia 90 kwamba hataongeza mchezaji mpya katika kikosi chake mnamo mwezi Januari. (BeInSports - via London Evening Standard)

Valencia imekubali dau la £31m kumsajili winga wa Paris St-Germain Goncalo Guedes.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa katika mkopo katika klabu hiyo ya Uhispania na amevutia Arsenal na Manchester United . (L'Equipe - via Sun)

Arsenal na Manchester City zinamkagua beki wa Burnley James Tarkowski, 25, kwa lengo la kumvutia katika dirisha la uhamisho la mwezi ujao.(Times - subscription required)

Mchezaji anayelengwa na Arsenal na Everton Steven N'Zonzi amedaiwa kuonekana katika uwanja wa ndege wa Gatwick.

Mchezaji huyo wa zamani wa Stoke na Blackburn 29, ameambia Sevilla kwamba anataka kuondoka.. (Sun)

Newcastle wanapigiwa upatu kumsajili mshambuliaji Islam Slimani, 29, kutoka Leicester. (Leicester Mercury)

Klabu hiyo pia imefanikiwa kumtia mkobani kwa mkopo winga wa Chelsea Kenedy, 21, na anatarajiwa kuwasili wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi ujao. (Daily Mail)

Ajenti wa kiungo wa kati wa Juventus Stefano Sturaro's anasema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye analengwa na Newcastle, huenda akahamia huko mwezi Januari. (Tribal Football - via Newcastle Chronicle)

West Brom itaangazia kumsajili beki wa Middlesbrough Ben Gibson iwapo itamuuza Jonny Evans, 29.

Klabu hiyo hatahivyo inakabiliwa na pingamizi kutoka kwa klabu hiyo ya daraja la kwanza kumnyakua mchezaji huyo mwenye umri wa 24-year-old. (Birmingham Mail)

Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere, 25, anasema kuwa anataka kusalia katika klabu hiyo na analenga kuichezea Uingereza katika kombe la dunia la 2018 (Sky Sports)

Liverpool itakataa katakata kumuachilia mshambuliaji Daniel Sturridge kuondoka mwezi Januari, na hivyobasi kuweka matumaini yake ya kutaka kuichezea Uingereza katika hali ngumu .

Newcastle, West Ham na Stoke zinamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 (Daily Mail)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amempatia Ben Woodburn ruhusa ya kuondoka katika klabu hiyo kwa mkopo.

Leeds United na Sunderland zinamwinda mshambuliaji huyomwenye umri wa miaka 18(Daily Express)

Mkurugenzi wa Inter Milan Walter Sabatini amesisitiza kwamba klabu hiyo haina nia ya kumuachilia Joao Mario, 24, kuondoka mwezi Januari.

Beki huyo amehusishwa na Manchester United and Paris St-Germain. (Independent)

Kipa Claudio Bravo, 34, amesema kuwa ana uhusiano mbaya na mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola lakini anasisitiza kuwa hana mpango wa kuondoka katika klabu hiyo hivi karibuni.(Goal.com)

Mada zinazohusiana