Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 22.12.2017

Henrikh Mkhitaryan hajawa chaguo la kwanza kwa José Mourinho kwa kipindi kirefu
Image caption Henrikh Mkhitaryan hajawa chaguo la kwanza kwa José Mourinho kwa kipindi kirefu

Inter Milan wameonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan kwa mkopo mwezi Januari, lakini bado hawajaweka wazi kama watamnunua moja kwa moja nahodha huyo wa Armenia.(Gazzetta dello Sport, via Talksport)

Swansea wako mbioni kumsajili mchezaji wa zamani wa Arsenal Dennis Bergkamp kuwa kocha wake baada ya Muholanzi huyo kutimuliwa kama meneja msaidizi wa Ajax.(Daily Express)

Kama mpango huo utashindikana, Swansea wanawasaka pia meneja wa zamani wa Crystal Palace Frank De Boer na Aitor Karanka aliyekuwa kocha wa zamani wa Middlesbrough.. (Times - subscription required)

Chelsea wana mpango wa kumfanya Thibaut Courtois kuwa mlinda mlango anayelipwa zaidi duniani kwa kumpa Paundi 200,000 kwa wiki, kwa sasa mazungumzo yanaendelea na Courtois raia wa Ubelgiji mwenye miaka 25.(Telegraph)

Image caption Thibaut Courtois amekuwa na kiwango kizuri tokea ajiunge na Chelsea

Manchester City wanaangalia hali ya mambo ya mlinzi wa AC Milani Leonardo Bonucci mwenye miaka 30 ambaye inasemekana hana raha katika klabu hiyo.(Gazzetta dello Sport - in Italian)

Kama mbadala City pia inamtupia jicho mlinzi kisiki wa Southampton, Virgil van Dijk, John Evans wa West Brom na Inigo Martinez wa Real Sociedad.(Telegraph)

Kiungo wa kati wa Barcelona na Hispania Sergio Busquets, yupo kwenye rada za Manchster City kwa dau la Paundi milioni 50 na Yaya Toure. (Daily Star)

Meneja wa Crystal Palace Roy Hodgson amesema hawezi kuwa na uhakika kama kiungo mshambuliaji wa timu ya Ivory Coast Wilfried Zaha atasalia katika timu hiyo wakati wa uhamisho wa mwezi Januari.(Reuters)

Kocha wa Everton Sam Allardyce anataka kumsajili mlinzi wa kati wa Crystal Palace James Tomkins kwa dau la paundi milioni 20.(Sun)

Mlinzi wa kati wa Sunderland Lamine Kone anaweza kujiunga na meneja wake wa zamani Sam Allardyce kunako klabu ya Everton mwezi Januari kwa paundi milioni 10.(Mirror)

West Ham inajiandaa kutoa dau la Paundi milioni 20 kwa mlinzi wa kati wa Swansea Alfie Mawson. (Guardian)

Meneja wa Stoke City Mark Hughes aha uhakika wa kuungwa mkono na klabu yake ili kuifanya kusalia kwenye ligi kuu ya EPL. (talksport)

Newcastle wameonyesha nia ya kumnasa mshambuliaji wa Leicester na Algeria Islam Slimani. (Leicester Mercury)

Image caption Kiwango cha Islam Slimani kwa sasa kinasuasua Leicester

Mshambuliaji wa Nice Mario Balotelli,27, anataka kuhamia timu kubwa na ameichagua Manchester City kwa uhamisho wa bure. (Daily Mirror)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anatarajiwa kuimarisha kikosi chake kwa kuongeza mshambuliaji mwezi Januari. (independent)

Manchester United wanamsaka kwa udi na uvumba kinda wa miaka 19 wa Borussia Dortmundand na Marekani Christian Pulisic. (Daily Mail)

Arsenal wanatarajia kumsajili kiungo mshambuliaji wa Barcelona Jose Arnaiz kwa ada ya Paundi milioni 20. (Marca)

Kiungo wa Barcelona Andres Iniesta amesema usajili wa Philippe Coutinho, 25, utakuwa muhimu zaidi Nou Camp. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Image caption Philippe Coutinho ni miongoni mwa wachezaji wanaoipaisha Liverpool kwa sasa

Liverpool inapambana na Borussia Dortmund kumpata beki kisiki wa Basel Manuel Akanji. (Independent)

Kiungo wa Atletico Madrid Nicolas Gaitan, ataondoka kwenye timu hiyo mwezi Januari baada ya timu mbalimbali za EPL kuonyesha nia kwa Muargentina huyo. (Foot Mercato, via Daily Mail)

Kiungo wa Stoke Stephen Ireland, 31, amekubali kutia saini mkataba mpya kunako klabu hiyo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii