Arsenal yatoka sare ya 3-3 na Liverpool EPL

Arsenal walikuwa nyuma 2-0 baada ya Phillipe Coutinho kufunga kwa kichwa naye Mohammed Salah akaongeza bao la pili katika kipindi cha pili. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsenal walikuwa nyuma 2-0 baada ya Phillipe Coutinho kufunga kwa kichwa naye Mohammed Salah akaongeza bao la pili katika kipindi cha pili.

Mshambulio kali la Roberto Firmino liliisaidia Liverpool kutoka nyuma na kupata sare katika mechi ya ligi ya Uingereza ambayo Arsenal ilifunga mabao matatu katika dakika tano za kipindi cha pili.

Arsenal walikuwa nyuma 2-0 baada ya Phillipe Coutinho kufunga kwa kichwa naye Mohammed Salah akaongeza bao la pili katika kipindi cha pili.

Lakini Arsenal iliimarika huku Alexis Sanchez akifunga kwa kichwa kufuatia krosi muruwa iliopigwa na beki wa kulia wa Arsenal Hector Bellerin kabla ya Granit Zhaka kufunga kombora la mbali ambalo lilimshinda kipa wa Liverpool Simon Mignolet.

Dakika mbili baadaye Mesut Ozil aliiweka kifua mbele Arsenal baada ya kufunga bao zuri kufuatia gusa ni guse na mshambuliaji wa Arsenal Lacazette.

Mchezo ulichezwa katika pande zote mbili za uwanja huku timu zote mbili zikionyesha hatari ya kutaka kufunga.

Lakini ilikuwa Liverpool iliosawazisha baada ya Firmino kuwachwa pekee katika safu ya Arsenal na kumfunga kipa Cech ambaye alishindwa kuupangua mpira huo na badala yake akaupungua na kuingia katika wavu wa goli lake.

Matokeo hayo yanaonyesha kuwa Liverpool imehifadhi nafasi yake katika jedwali la ligi huku nayo Arsenal ikisalia katika nafasi ya tano ikiwa nyuma ya Liverpool kwa pointi moja.

Mada zinazohusiana