Je Messi atamfunga mdomo mchezaji bora dunia Ronaldo 'El Clasico'?

Mchezaji bora duniani Cristiano Ronaldo na aliyeuwa mchezaji bora Lionel Messi wa Barcelona
Image caption Mchezaji bora duniani Cristiano Ronaldo na aliyeuwa mchezaji bora Lionel Messi wa Barcelona

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo na winga Gareth Bale wote wako asilimia 100 tayari kucheza katika mechi kali zaidi duniani ya ''El Clasico'' dhidi ya Barcelona baada ya kupata majeraha kulingana na mkufunzi Zinedine Zidane.

Raal Madrid ambao wako katika nafasi ya nne wako pointi 11 nyuma ya viongozi wa ligi ambao hawajashindwa Barcelona.

''Ronaldo alifanya mazoezi pekee mapema wiki hii, akiwa na jeraha la shavu la mguu, lakini alifanya mazoezi vizuri siku ya Ijumaa huku Bale naye akiendelea kupona jeraha la shavu la mguu.Yuko salama yuko asilimia 100'' .

''Amefanya mazoezi leo'', Zidane alisema kuhusu Ronaldo.

Bale hajacheza katika liga ya la Liga tangu mwezi Septemba, lakini aliwekwa mara mbili katika benchi katika kombe la dunia la vilabu , ambalo Real ilishinda.

''Sitachagua mchezaji kwa saababu nataka acheze katika El Clasicco'', alisema Zidane.

''Ninawaamini wachezaji wangu na wanaweza kupata majeraha, lakini kitu muhimu ni kwamba yuko asilimia 100 tayari kucheza.Tutaona iwapo atacheza ama la.''

''Barca haijapoteza mechi ya la liga msimu huu chini ya kocha Ernesto Valverde'', alisema kuwa:

''Sidhani kwamba sisi ndio tunapigiwa upato kushinda, jedwali la ligi halina ushawishi wowote wa mechi kama hizi kutokana na wasiwasi uliopo kila mara''.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kocha wa Barcelona Valverde na Zinedine Zidanne wa Real Madrid

''Madrid ni timu yenye uwezo mkubwa ambayo inaweza kukuangusha wakati upo katika hali nzuri kabisa .Pia watakuwa nyumbani'''.

Zidane hafiriki kwamba iwapo watashindwa basi timu yake itapoteza matumaini kutetea taji lao.''hatujafikiria kuhusu tofauti ya pointi''.

''Sidhani kama ni mechi ambayo itaamua chochote katika ligi. Lazima uwe na motisha .Sisi ni wazuri katika kila safu ya uwanja.Hata iwapo tutapoteza ushindani wa ligi haujakwisha''.

Mada zinazohusiana