Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 24.12.2017

Luke Shaw Haki miliki ya picha Empics
Image caption Luke Shaw

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anasema yuko tayari kutoa afa mara mbili kwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Everton Ross Barkley, 24, na mlinzi wa Manchester United Luke Shaw, 22. (Sunday Express).

Manchester United wamekawaia kumpa Mourinho mkataba mpya wakati Man U ikishuka katika ligi. (Mirror).

Ajenti wa Olivier Giroud atasafiri kwenda London wiki hii kwa mazungumzo kuhusu hatma ya mshambuliaji huyo wa Arsenal wa miaka 30. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jack Wilshere

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal, Jack Wilshere, 25, yuko kwa orodha kwenye orodha ya kombe la dunia yake Gareth Southgate baada ya kurudi katika kikosi cha kwanza cha Gunners. (The Sun)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anammezea mate mchezaji wa safu ya kati wa Shakhtar Donetsk, Fred 24 wakati City wanataka kuimarisha kikosi chao msimu ujao. (Mail on Sunday)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Henrikh Mkhitaryan

Arsenal wamepiga hatua mbele ya Manchester United na Chelsea katika mbio za kumpata wing'a wa Bayer Leverkusen Leon Bailey 29. (Mirror)

Inter Milan wanataka kuchukua mchezaji wa safu ya kati wa Henrikh Mkhitaryan, 28, kwa mkopo kutoka Manchester United. (Mail on Sunday)

Bournemouth imekataa ofa kutoka kwa West Ham ya pauni milioni 8 kwa mchezaji wa miaka 27 Harry Arter. (Sunday Express)

Mada zinazohusiana