Mshambuliaji wa Southampton Charlie Austin apigwa marufuku ya mechi tatu

Charlie Austin and Jonas Lossl Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji wa Southampton Charlie Austin apigwa marufuku ya mechi tatu

Mshambuljia wa Southmpton Charlie Austin amepigwa marufuku ya mechi tatu na shirika la kandanda la FA kwa kucheza vibaya.

Austin alimpiga kiatu kipa wa Huddersfield Jonas Lossl, usoni wakati wa mechi ya Jumamosi ambapo walitoka sare ya 1-1.

Mfungaji huyo bora wa Southampton mwenye umri wa miaka 28, ambaye amefunga mabao 6 msimu huu atakosa mechi dhidi ya Tottenham, Manchester United na Crystal Palace.

Alipata jeraha na kuondolewe uwanjani dakika ya 79.

Meneja wa Southampton Mauricio Pellegrino alisema kuwa jeraha hilo litamweka nje Austin kwa wiki kadhaa.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Kuhusu BBC

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea