Serena Williams kurudi uwanjani miezi minne baada ya kujifungua

Serena Williams Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Serena Williams kurudi uwanjani miezi minne baada ya kujifungua

Nyota wa tenisi Serena Williams atarejea uwanjani huko Abu Dhabi wiki ijayo miezi minne baada ya kujifungua.

Serena mwenye umri wa miaka 36, atakutana mchezaji nambari saba duniani Jelena Ostapenko tarehe 30 Disemba wakati wa mechi ya ubingwa wa dunia ya Mubadala

Alijifungua mtoto msichana Alexis Olympia Ohanian mwezi Septemba.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bingwa huyo wa zamani duniani hajacheza tangu alisema Australian Open mwezi Januari.

Bingwa huyo wa zamani duniani hajacheza tangu alisema Australian Open mwezi Januari.

Mkurugenzi wa Australian Open, Craig Tilley amesema kuwa Williama anatarajiwa kutetea taji lake katika mechi ya mwaka 2018 ambayo itaanza Januari 15.

Rafael Nadal, Milos Raonic na Stan Wawrinka wamejiondoa kutoka kwa Mubadala ambayo itachezwa kati ya 28-30 Disemba.

Mada zinazohusiana