Harry Kane aweka rekodi ya mabao mengi kwa mwaka EPL

Harry Kane aweka rekodi ya mabao mengi kwa mwaka EPL
Image caption Harry Kane aweka rekodi ya mabao mengi kwa mwaka EPL

Harry Kane amefunga hat-trick na hivyobasi kuweka rekodi mpya ya mabao mengi yaliofungwa kwa mwaka huku Tottenham ikiicharaza Southampton katika uwanja wa Wembley.

Mshambuliaji huyo wa Spurs na Uingereza alifunga bao lake la 37 la mwaka 2017 katika dakika ya 22 na hivyobasi kuipiku rekodi ya Alan Shearer iliowekwa wakati alipokuwa akiichezea Blackburn 1995.

Kane baadaye aliongeza mabao mengine mawili katika vipindi vyote viwili na kufanya jumla ya mbao aliyofunga kwa klabu na taifa kuwa 56 mawili zaidi ya mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi.

Kabla ya bao la tatu la Kane, Dele Alli alikuwa amefanya matokeo kuwa 3-0 katika dakika ya 49 wakati alipocheka na wavu na dakika mbili baadaye akampatia Son Heung-min ambaye alimfunga kipa Fraser Forster.

Southampton ikicheza bila mfungaji wake mkuu Charlie Austin ilijipatia bao lake la kwanza kabla ya Dusan Tadic kuongeza la pili.

Licha ya kuimarika katika kipindi cha pili , Southampton haikuweza kuharibu sherehe ya Tottenham na sasa wamecheza miezi miwili bila ushindi.

Wakati huohuo Spurs imeipiku Liverpool katika nafasi ya nne huku The Reds wakicheza dhidi ya Swansea siku ya Jumanne.

Akizungumza kuhusu rekodi yake ya miaka 22 iliyovunjwa, Shearer alituma ujumbe wa Twitter akisema: Umekuwa na mwaka mzuri sana wa 2017 .Unahitaji kuchukua rekodi hiyo ya mabao mengi katika ligi ya uingereza katika mwaka mmoja . Kongole na enedelea na kazi nzuri.

Mada zinazohusiana