Man United yalazimika kupigania sare ya 2-2 dhidi ya Burnley

Jose Mourinho alionekana kujaa wasiwasi wakati mechi hiyo ilipoendelea Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jose Mourinho alionekana kujaa wasiwasi wakati mechi hiyo ilipoendelea

Manchester United imelazimika kupigania sare ya 2-2 dhidi ya Burnley baada ya kutoka nyuma nyumbani.

Burnley ilikuwa ya kwanza kufunga katika kipindi cha pili kupitia Burnes dakika ya 3 na Defour kunako dakika ya 36.

Hatahivyo Man United ilicheza kufa kupona na kupata bao lake la kwanza kupitia mchezaji Jesse Lingaard kunako dakika ya 53 wakati wachezaji wa Burnley walipokuwa wakijaribu kutetea mabao yao.

Jesse Lingard aliongeza bao la pili katika dakika za lala salama ambapo Man United iliwalemea wageni wake katika safu zote na kulazimika kurudi nyuma.

Matokeo hayo hatahivyo yanaihakikishia Man United nafasi yake ya pili.

Mada zinazohusiana